Samia akoleza moto Taifa Stars, Kocha akoshwa

MARRAKECH,Morocco: Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Adel Amrouche amesema kitendo cha Rais Samia Suluhu Hassan kutoa ndege kwa ajili ya timu hiyo kinawapa ari ya kupambana zaidi ili kupata matokeo katika michezo iliyo mbeleni.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini Morocco tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Niger, kocha huyo amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuunga mkono michezo na kwamba wanajihisi wenye deni na wapo tayari kuipeperusha vyema bendera ya taifa katika michezo yao.
Stars inaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Grand Marrakech Annex1 wakisubiri kuivaa Niger katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kombe la dunia 2026 mwaka utakaopigwa mjini Marrakech Morocco Novemba, 18,2023.
 
Ndege iliyotolewa na Rais Samia itaisubiri timu hiyo ili kuirudisha nyumbani mapema kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa pili dhidi ya Morocco utakaopigwa Novemba 21 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
15 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions….
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Last edited 15 days ago by Angila
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x