Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa kuwajengea mazingira mazuri vijana ya kupata mikopo nafuu.
Pia vijana hao nao wametakiwa kukopa kwenye Taasisi za Fedha zinazolenga kuwainua kiuchumi, badala ya zile zinazotaka kuwatumia kujiongezea mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi ambaye pia ni Mwanzilishi wa Yes-Vicoba, Happy Lyaruu amebainisha kuwa Rais Samia amezijengea mazingira mazuri Taasisi za Fedha kufanya kazi hatua inayowawezesha kukopesha vijana.
Amesema kwa sasa vijana wanao mwanya mpana zaidi wa kukopa na tena mikopo haiumizi.
Happy anasema kuwa vijana wanatakiwa kupatiwa huduma nafuu za mikopo, ambazo zitawawezesha kujiinua kimaisha badala ya kuwapatia mikopo inayogeuka kuwa mzigo utakaowazuia kujihusisha kwenye shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.
Anasema Yes- Vicoba, inaamini kuwa iwapo vijana wakipatiwa mikopo nafuu watakuwa kwenye nafasi nzuri za kulima aina mbalimbali za mazao yakiwemo ya biashara na kuyauza ndani na nje ya nchi na kuwa Yes- Kikoba kimejipanga kuwapatia mikopo hiyo.
“Yes- Vicoba ni huduma ya kukopesha bila riba ambapo kijana anapewa mkopo itakayoendana na ushairi wa kibiashara, yani wanapatiwa elimu ya biashara kwanza ikiwa ni pamoja na kufundishwa mbinu zote za biashara ikiwa pamoja na kupewa ushairi wa aina gani ya biashara ya kufanya,”alisema Happy.
Anasema kuwa Yes- Vicoba itawasaidia vijana kunufaika na kilimo kwa kutumia mikopo yake anasema:” Nitaanzisha tawi maalumu la BBT-VICOBA ambapo vijana wataweka hisa zao na kupata mikopo isiyokuwa na riba kuanzia 1,000,000 hadi 10,000,000, bila ya kutoa dhamana yoyote, wanachama watadhaminiana wao kwa wao,” aliongeza.
Anasema, kwa kuwa mradi wa BBT unalenga kuwawezesha vijana katika kilimo ambapo watakuwa wakilima aina mbalimbali za mbogamboga na watakuwa na soko la uhakika la kuuza bidhaa zao zitokanazo na kilimo hatokuwa na wasiwasi kuwasaidia.
Comments are closed.