Samia ampa tano RC mpya Tabora

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ndio sababu iliyompa nafasi ya kuaminiwa zaidi na kupandishwa cheo.

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi walioteuliwa hivi karibuni uliofanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Rais amesema Tamisemi wameanza utaratibu wa kupima viwango vya utendaji kwa watumishi ili kujua nani anafanya nini katika nafasi yake.

“Kwa mujibu wa tathimini iliyofanywa na Tamisemi Chacha ulionekana kufanya vizuri sana na ndio maana tumeona tukupandishe kutoka kuwa mkuu wa wilaya hadi mkuu wa mkoa”amesema Rais Samia

Rais Samia amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuzimaliza changamoto zilizopo mkoani Tabora kwani hana ugeni na mkoa huo. Amesema akasimamie vyema mazao ya kilimo kwani mkuo huo ni wazalishaji wazuri wa mazao hayo.

Ikumbukwe kabla ya uteuzi huo Chacha alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button