DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amemwagia sifa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda akisema kiongozi huyo amefanya kazi kwa ubora mkubwa katika nafasi alizohudumu.
Akihutubia baada ya uapisho wa viongozi leo Ikulu Dar es salaam Rais amesema Makonda amefanya kazi nzuri akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM , naye kama Mwenyekiti wa Chama hicho anajivunia kile alichokifanya.
“Paul (Makonda) umefanya kazi nzuri CCM, umekichemsha chama,” na umefanya kazi nzuri ukiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema Rais Samia
“Tumekupeleka Arusha, unajua nini kipo Arusha. Nina Imani unajua nini chakufanya, nina Imani na wewe” amesema Rais Samia