RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hasaan amemteua Stephen Wassira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), kwa kipindi cha pili cha miaka minne baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 25, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, imeeleza kuwa Rais Samia pia amemteua Dk Fedelice Mbaruku Simbangulile Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia Aprili 3, 2023.