Samia apongezwa Royal Tour kuongeza ajira

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema ushiriki wa Rais Samia Suluhu Hassan katika uandaaji na uzinduzi wa filamu ya Royal Tour umewezesha vijana wengi kupata ajira kutokana na ongezeko la watalii.

Profesa Ndalichako alisema hayo Dar es Salaam alipokuwa akizindua hafla ya ugawaji wa tuzo ya Vijana Chipukia Tanzania.

Alisema jambo hilo limedhihirisha kuwa Rais Samia ameendelea kutafuta fursa mbalimbali nje na ndani ya nchi ili kuweza kuvutia wawekezaji nchini na hatimaye kuongeza ajira nchini.

Pia alisema katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi vijana, serikali imeendelea kuwawezesha kwa kutoa mikopo ya kiasi cha Sh bilioni 14.51 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri.

“Ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa mikopo, wizara imeboresha mwongozo wa utoaji wa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kupitia mwongozo huo, muda wa maresho umeongezwa kutoka miezi 24 hadi 36.

“Aidha, wigo wa utoaji mikopo umeongezeka kwa kujumuisha kampuni, viwanda na kijana mmoja mmoja. Pia vyanzo vya mapato vya mfuko vimeimarishwa kwa kujumuisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za umma, watu binafsi na wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Africa Youth Transformation, Justine Mponda akizungumzia tuzo hizo alisema lengo ni kutambua mchango wa vijana katika sekta za uchumi na namna ambavyo wanaleta ubunifu katika kutatua changamoto katika jamii.

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x