Samia ataja Mikoa vinara mimba za utotoni
DAR ES SALAAM: Wakati Tanzania ikiendelea na mapambano dhidi ya mimba za utotoni kuna baadhi ya mikoa bado changamoto hiyo ipo kwa kiasi kikubwa hivyo kutia doa harakati za mapambano hayo.
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam leo, Oktoba 28, 2023, amesema
Ripoti hiyo imeonesha mikoa inayoongoza mimba za utotoni ni Songwe asilimia 45, Ruvuma asilimia 37, Katavi asilimia 34, Mara asilimia 31 na Rukwa asilimia 30.
Kiongozi huyo wa nchi amesema mikoa ya Dodoma, Kigoma, Tabora na Shinyanga imefanikiwa kupunguza mimba za utotoni na kwamba mikoa hiyo inahitaji pongezi.” Ameongeza.
Sote tunao wajibu wa kulinda maisha ya watoto wetu tutimize wajibu wetu, ripoti hii inaonesha kumekuwa na mafanikio katika kupunguza mimba za utotoni kutoka asilimia 27 mwaka 2015/2016 hadi asilimia 22 mwaka 2022, tumepunguza asilimia 5,” amesema Rais Samia.
Pia Rais Samia amewataka viongozi kutoka mikoa yenye idadi kubwa ya mimba za utotoni kujitathimini na kufahamu sababu ya ukubwa wa tatizo hilo katika maeneo yao.
Ametolea mfano Mkoa wa Dar es Salaam amesema mimba za utotoni zimeongezeka kutoka asilimia 11.9 hadi 18.1.
“Mkoa wako (wa Dar es Salaam), Albert Chalamila mmerudi nyuma…mmelegeza wapi sjui, kajiangalieni muwalinde watoto wenu. mmelegeza wapi sjui?” amehoji.