Samia atajwa ushindi Taifa Stars

DAR ES SALAAM: RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amesema mafanikio ya timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ‘Taifa Stars’ yamechagizwa na hamasa inayotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema hayo alipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kuipokea Taifa Stars, iliyowasili nchini ikitokea Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 dhidi ya Niger hapo jana na kuibuka na ushindi wa 0-1.

Karia amesema Rais ametoa ndege kuisafirisha Stars, hali inayowafanya warejee nyumbani kwa wakati, na kupata muda wa kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 21, 2023.

Kwa upande mwingine, Karia amesema kutokana na mazingira rafiki ya kinchi na hali nzuri za viwanja nchini, Tanzania inapokea timu nyingi za taifa zikitumia viwanja vilivyopo kama viwanja vyao vya nyumbani.

“Kama ulikuwa hufahamu, mpaka sasa kuna timu tano za taifa zipo hapa nchini, ikiwemo Burundi, Gambia, Gabon, Ivory Coast pia Morocco.” Amesema Karia

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
MONEY MARKER
MONEY MARKER
18 days ago

Mbunge wa KWANZA MZUNGU KWENYE BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA… KUWAKILISHA HELA ZA WORD BANK, IMF, MISAADA KUTOKA ULAYA… N.K – ZA KUJENGEA BARABARA, RELI, FLYOVER,

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

HELA ZAO HAZINA MWAKILISHI – KAMA FUNDI ANAHITAJI NYUMBA YAKE KWA SABABU ALIJENGA YEYE (MCHANGA KANIPA HELA)

Melissick
Melissick
18 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 18 days ago by Melissick
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x