Samia ataka uwekezaji rasilimali watu

RAIS Samia Suluhu Hassan amezindua mchakato wa maandalizi ya mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika, kuhusu maendeleo ya rasiliamli watu utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 25 hadi 26 mwaka huu.

Akizindua mchakato huo, Rais Samia amesema viongozi wa Afrika wanapaswa kuwekeza kwenye rasilimali watu ili kuharakisha ukuaji wa uchumi, kuongeza tija kwa vijana na wanawake kwa kuboresha mafunzo na ujuzi.

Amesema ni muhimu kwa viongozi wa Afrika kuwekeza kwenye rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi barani Afrika kama kauli mbiu yam waka huu inavyosema ‘kuharakisha ukuaji wa uchumi wa Afrika, kuongeza tija kwa vijana kwa kuboresha mafunzo na ujuzi’ hiivyo ni fursa kwa wakuu wa nchi kujadili na kubadilisha uzoefu kuhusu mchango wa rasilimali watu katika ukuaji wa uchumi na maendeleo.

“Afrika bado haijawekeza vya kutosha kwenye rasilimali watu hususani chini ya Jangwa la Sahara, ni muhimu kwetu viuongozi kuendelea kuwekeza kwa watu husani vijana na wanawake kwa kuhakikisha sera zinazotungwa zinaimarisha ubora na uwezo wa watu wao.”Amesema

Amesema, kwa mujibu ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) zinazohusiana na maendeleo ya rasilimali watu japo Tanzania imeanza kuchukua hatua na inaendelea vizuri.

“Tanzania tayari tumeshaanza, tumechukua hatua mbalimbali katika kutekeleza SDGs, tunasonga mbele, tunachohitaji ni kuungwa mkono, tutatoa taarifa za kina wakati wa mkutano mwezi Julai,”amesema Rais Samia na kuongeza

“Kwa Tanzania maendeleo ya rasilimali watu ni moja ya vipaumbele vyetu muhimu katika mipango yetu yote ya maendeleo.Tumefanya kazi nzuri na tunaendelea, tunahitaji kuungwa mkono ili tuende vizuri na kwa wepesi.”

Amesema, ajenda ya 2063, Afrika imeweka hoja ya kuwa na rasilimali watu yenye tija kama moja ya ajenda zake muhimu, hivyo wanahitaji kuwekeza katika elimu na afya kwa wote, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na kuwekeza kwenye ujuzi muhimu unazohitajika kwa Afrika kukua kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button