RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka waumini wa kiislamu kuendelea kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, @SuluhuSamia, Rais Samia amewaasa waumini hao kuomba kwaajili ya amani, upendo, mshikamano, utulivu na haki akisema akizitaja kuwa nguzo za kustawisha maendeleo.
“Nawatakia Waislamu wote Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Katika mwezi huu wa ibada na toba tuendelee kuiombea nchi yetu amani, upendo, mshikamano, utulivu na haki; nguzo zenye kuleta ustawi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu. Ramadhan Kareem,” aliandika Rais Samia.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally jana alitangaza kuwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza leo, Alhamisi Machi 23, 2023.