Samia atoa maelekezo TTCL, NDC

RAIS Samia Suluhu amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), liachane na biashara ya simu, huku akilitaka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) lijitathmini.

Akizungumza leo Machi 29, 2023 mara baada ya kupokea ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), Charles Kichere na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Salum Hamduni, Rais Samia amesema ni wazi kuwa TTCL biashara ya simu imeshindwa, wakati NDC limekuwa likijiendesha kwa hasara miaka nenda rudi.

Akizungumzia TTCL, Rais Samia amesema: “ TTCL biashara ya simu imeshindwa, mkongo wa kwao kwanza hakuna fairground tuitazame, wasimamie makampuni ya simu lakini sio wao kujiingiza kwenye simu, wafanye kitu kingine wanachokiweza.”

Akilizungumzia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Rais Samia amesema kuna mashirika hayafai kuwepo, yamepitwa na wakati na hayajawahi kuwa na impact yoyote miaka mingi sasa.

“Bila ya kigugumizi shirika la NDC kwa wale wa umri wangu toka tunatumia sabuni ya life boy kutoka nje, na betri zetu za national  tunatengeneza hapa, mimi nilikuwa sekondari mpaka leo nipo kwenye kiti hiki.

“Ukitafuta ripoti ya NDC lini walifanya ‘positive impact’ utakuta labda awamu ya kwanza ile walipoundwa, lakini si ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano si hii, lakini dude kama NDC lipo..lipo..kuna wengi kama NDC.

“Kawaangalieni, haya mashirika yanakula tu pesa  kutoka serikalini yenyewe hayaleti, madhumuni ya kuunda mashirika yakafanye biashara kwa niaba ya serikali yakalete pesa lakini hayaleti.

“Kila mwaka bajeti ya mashirika iko hapo, wafanyakazi wa mashirika tunalipa, magari ya mashirika yanatumia cost serikalini kila kitu, lakini yenyewe hayachumi kuleta huku, kama yanachuma yanafaidisha wengine lakini si serikali.

“Yafanyieni tathmini, mashirika 300 sijui 200 ya nini, yafanyieni tathmini yale yanayofaa yawekwe, yasiyofaa yafutwe …. Wafanyakazi watawekwa tu huko kunakoombwa ajira kila siku… mashirika yaangaliwe, sio kwa faida yangu kwa faida ya nchi,” amesisitiza.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button