Samia awapa CTI mbinu ya ushindi

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka wazalishaji wa bidhaa kupitia Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kuimarisha ubora wa bidhaa wanazozalisha nchini.

 

Rais Samia amesema hayo mwishoni mwa juma wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Aidha, Rais Samia amesema Serikali imeimarisha miundombinu ya barabara na bandari ili bidhaa zinazozalishwa zisafirishwe nje na kuingia nchini ili sekta ya viwanda iendelee kufanya vizuri.

Rais Samia pia amewataka wazalishaji hao kuongeza juhudi katika uzalishaji na uongezaji wa bidhaa (intermediate goods) ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Hali kadhalika, Rais Samia amesema mbali ya kukua kwa sekta ya utalii, jitihada nyingine
inayofanywa na serikali kudhibiti dola ni kujishughulisha na kilimo hasa cha muda mfupi
ambacho kinazalisha mazao kwa haraka.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button