Samia awapangia vituo mabalozi wateule

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi mabalozi wateule sita aliowateua Mei 10, 2023 na amewabadilisha vituo mabalozi wanne, huku akimrudisha nyumbani Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri.

Mabalozi aliowapangia vituo vya kazi ni Balozi Fatma Mohamed Rajabu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Omani akichukua nafasi ya Balozi Abdallah Kilima ambaye amestaafu.

Balozi Joseph Sokoine amekua Balozi wa Tanzania nchini Canada akichukua nafasi ya Balozi Dkt Mpoki Ulisubisya ambaye amestaafu. Balozi Naimi Hamza Azizi amepangiwa kuwa Balozi nchini Austria.

Advertisement

Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi

Meja Jenerali Ramson Mwaisaka ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Meja Mwaisaka anachukua nafasi ya Balozi Meja Richard Makanzo ambaye amehamishiwa Cairo Misri.

Aidha, Gelasius Byakanwa Balozi mteule nchini Burundi akichukua nafasi ya Balozi Jilly Maleko ambaye amestaafu, huku Habibu Awesi Mohamed akipangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Qatar. Habibu anachukua nafasi ya Balozi Mahadhi Juma Maalim ambaye amehamishiwa Kuala Lumpur, Malaysia.

Imani Njalikai ameteuliwa kwua Balozi wa Algeria, Njalikai anachukua nafasi ya Meja Jenerali Jacob Kingu ambaye amestaafu.

Hassan Idd Mwamweta amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujeruamani, Mwamweta anachukua nafasi ya Balozi Abdallah Saleh Posi ambaye amehamishiwa Geneva, Uswis, Dkt Mohamed Juma Abdallah Balozi mteule nchini Saudi Arabia akichukua nafasi ya Balozi Jabir Mwadini ambaye amehamishiwa Paris, Ufaransa.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema iliyotolewa leo Agosti 11, 2023 inasema kuwa wateuliwa wote wataappshwa Agosti 16, 2023 saa tano kamili asubuhi, Ikulu Chamwino mjini Dodoma.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *