Samia awasili KIA akielekea Monduli

KILIMANJARO; Rais Samia Suluhu Hassan amewasili Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro KIA,tayari kwa ajili ya kuelekea wilayani Monduli mkoani Arusha kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Rais Samia amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda na  Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Rais Samia anatarajiwa kuungana na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali kwenye kumbukizi hiyo inayofanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine, kijijini Enguiki wilayani Monduli.

Habari Zifananazo

Back to top button