Samia azuia vibali 125 kulinda Bonde la Rufiji

BODI ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji (RBWB) imezuia vibali 125 vya shughuli katika Bonde la Rufiji kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais alitoa agizo hilo Desemba mwaka jana wakati akizindua uingizaji maji katika bwawa la kufua umeme kwa kutumia maji la Julias Nyerere (JNHPP).

Akizungumza na HabariLEO jana, mkuu wa kitengo cha ugawaji rasilimali za maji katika bonde hilo. Gallus Ndunguru alisema katika kikao cha bodi kilichofanyika Januari mwaka huu walifikia maamuzi ya kusitisha utoaji vibali kwa miradi mikubwa.

Ndunguru alisema kati ya vibali hivyo vilivyozuiwa, vingi ni kuomba kuwekeza katika mashamba ya umwagiliaji na lengo ni kuhakikisha wanaruhusu maji kujaza bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema kuzuia shuguhuli katika bonde zinasaidia kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha mito midogo na mikubwa inatiririsha maji ya kutosha kuingia katika bwawa hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button