Samia: Chongolo unaijua vizuri Songwe

Rais Samia Suluhu Hassan

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan amesema anaamini Mkuu mpya wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo anakwenda kuzimaliza changamoto zilizopo mkoani hapo kwani kiongozi huyo anaufahamu fika mkoa huo.

Samia amezungumza hayo leo kwenye hafla ya uapisho wa viongozi walioteuliwa hivi karibuni uliofanyika Ikulu Dar es Salaam nakusema Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chama cha Mapinduzi CCM anafahamu changamoto za Songwe.

“Tunakupeleka Songwe kwasababu unaijua vizuri unaijua ukiwa chamani na imani yangu ni kwamba utakwenda kuusimamia vizuri” amesema Rais Samia na kuongeza

Advertisement

“Songwe inatuunganisha na Zambia, kuna Tunduma pale ambapo mambo mengi ya kiuchumi yanatokea na kuna uharibifu wa uchumi unafanyika ukiwemo ukwepaji wa kodi, ubadilishanaji wa fedha usio halilali na mambo mengine, nenda kasimamie vizuri pale. Amesema Samia.

 

 

/* */