Samia: Dk Salim ni Mtanzania mahiri

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan, amesema tovuti ya Dk. Salim Ahmed Salim, ni hazina kubwa kwa taifa letu, ina manufaa kwa wale wote wanaotaka kujifunza, masuala ya kidiplomasia na uongozi.

Dk. Samia ameyasema hayo leo Septemba 30, 2023 katika uzinduzi wa tovuti ya kwanza ya hifadhi ya nyaraka ya Kiongozi kwa njia ya kidigitali inayotambulika  “The Salim Ahmed Salim Digital Archive” www.salimahmedsalim.com katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

“Nimefarijika sana kusikia tovuti hii itakuwa endelevu na itakuwa ikiboreshwa mara kwa mara,”

Aidha, Dk. Samia amesema kupitia ushirikiano wa serikali na familia ya Dk. Salim, tovuti hii itamuwezesha kila mmoja kuifikia bila gharama yeyote.

“Tunapomzungumzia Dk. Salim Ahmed Salim, ni ukweli usiopingika kwamba huyu ni Mtanzania mahiri,

“Katika nyanja ya kidiplomasia Dk. Salim alituwakilisha katika nchi mbalimbali ikiwemo Misri, India, China,

“Dk. Salim alichapa kazi kwa moyo wake wote hivyo kudhihirisha uadilifu na uchapakazi,” Dk.

Samia amenukuliwa.

Habari Zifananazo

Back to top button