Samia: Geay, Simbu wameliheshimisha taifa

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amemtakia heri mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Gabriel Geay katika mbio za Boston Marathon 2024 leo nchini Marekani.

Akiwasilisha salamu hizo za Rais, katika mkutano na waandishi wa Habari mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameeleza kuwa mwanariadha huyo ameiletea heshima nchi. mwaka jana alimaliza wa pili katika mbio hizo .

Katika Boston Marathon mwaka jana Geay alitumia saa 02:06:04 huku akiwapita wanariadha kadhaa nguli duniani, katika mbio mbio ambazo Mkenya, Vans Chebet aliyetumia saa 02:05:54 aliibuka mshindi.

Matinyi amesema Rais Samia pia amempongeza mwanariadha mwingine wa Tanzania, Alphonce Simbu kwa kumaliza wa pili katika Daegu Marathon za nchini Korea Kusini kwa kutumia saa 2:07:55 na kuondoka na mamilioni ya shilingi.

Geay ni mmoja wa wanariadha wanne wa marathoni wa Tanzania waliofuzu kwa Michezo ya Olimpiki 2024 itakayofanyika Paris, kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11 nchini Ufaransa.

Habari Zifananazo

Back to top button