RAIS Samia Hassan Suluhu, anatarajia kufungua maonesho ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayotarajia kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 19, mwaka huu.
Pia maonesho hayo yanaenda sanjari na kongamano la siku mbili linaloanza kesho na kushirikisha washiriki zaidi ya 300, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Profesa Joyce Ndalichako atafungua kongamano la siki mbili Mei 16 hadi 17,mwaka huu.
Akizungumza na waaandishi wa habari leo , jijini Arusha, Dk Adolf Rutayuga, ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu Maonesho ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kwa nguvu kazi mahiri “, yatashirikisha washiriki na wajasiriamali zaidi 150.
Lengo nia kueleza umma vyuo vya ufundi stadi vinafanya nini, ili wazazi walezi wajue wafanye uchaguzi upi wa kupeleka watoto vyuoni, ili kuinua ustadi na kusaidia vyuo na walimu, ili waweze kukuza ujuzi wao na kujiajiri wenyewe.
“Rais Samia atazindua maonesho hayo Mei 19 mwaka huu, lakini tutakuwa na kongamano kwa ajili ya kuwajengea vijana ujuzi ili waweze kujiajiri,” amesema.
Anasema kuna mabadiliko ya mitaala katika vyuo vya ufundi lengo waweze kutenda kazi kwa mikono, hivyo lengo la vyuo vya ufundi ni kuzalisha vijana wengi zaidi, ili waweze kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa