Samia kuzindua Hospitali ya Rufaa Chato

RAIS Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Geita, kuanzia Oktoba 15 hadi 16, 2022, ambapo akiwa mkoani hapa atazindua Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, ametoa taarifa hiyo leo kwa waandishi wa habari na kueleza Rais Samia atawasili mkoani Geita kupitia wilayani Chato, akitokea mkoani Kagera.

Alisema pia atakagua na kuzindua mradi wa Kituo Kikuu cha Kupozea Umeme Mpomvu mjini Geita na mradi wa kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Geita (GGR) na kisha kwenda kuzungumuza na wananchi Uwanja wa CCM Kalangalala.

Shigella aliwaomba wananchi kumlaki Rais Samia, kwani ndani ya muda mfupi mkoa umepokea zaidi ya Sh bilioni 190, ili kutekeleza miradi mbalimbali.

 

Habari Zifananazo

Back to top button