Samia: Maktaba imeungua

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Rais wa awamu ya pili, hayati Ali Hussein Mwinyi alikuwa mwanamageuzi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii ambaye aliyeheshimu haki za watu na utawala bora.

Akizungumza wakati wa shughuli za mazishi katika uwanja wa Amaan, Rais Samia amesema Mwinyi alisimamia mageuzi ya kisiasa kwa kurejesha mfumo wa vyama vingi pia aliruhusu uwekezaji kutoka kwa kampuni binafsi.

Rais Samia ametaja mafunzo aliyopata kwa Mwinyi kuwa ni kiongozi shupavu asiyeyumba kwani licha ya masharti magumu ya sera za kiuchumi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) pamoja na kuwa na uchumi dhaifu ila Mwinyi alifanya mageuzi makubwa.

Advertisement

Amesema Mwinyi alikuwa ni maktaba inayotembea na iliyosheheni vitabu vyenye mafunzo ya uadilifu, uzalendo, ustahaimilivu, mageuzi, ujasiri, unyenyekevu na uchamungu.