RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake wa Chadema (BAWACHA) kitaifa itakayofanyika mkoani Kilimanjaro Machi 8, 2023.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hayo leo Machi 5, 2023 alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, ambapo ameeleza kuwa lengo la kumualika Rais Samia ni kusikiliza changamoto za Bawacha na kuzifanyia kazi.
“Tutampokea na kumkaribisha, tutamweleza changamoto, lakini akina mama nyie ndio mtamweleza changamoto rasmi za chama chetu au za siasa za upinzani,” amesema Mbowe.