DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Maridhiano Tanzania Machi 6, 2024, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania (JMAT).
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Alhad Mussa Salum, amesema pia siku hiyo kutakuwa na upandaji miti na uchangiaji damu na kutoa wito kwa wadau wa amani nchini kujitokeza kwa wingi.
Pia jumuiya hiyo imekiomba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiachane na mpango wake wa kufanya maandamano katika mikoa mbaimbali wakati huu, ambapo Taifa lipo katika majonzi ya kuondokea na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
Akizungumzia hilo, Mchungaji Christopher Kalata,ambaye ni mjumbe kwenye jumuiya hiyo amesema kufanyika kwa maandamano hayo si utu, wala hekima kutokana na wakati mgumu uliopo, huku Father Johson Lameck akiomba chama hicho kitumie wakati huu kushikamana,kujenga nchi na kuimarisha upendo.