Samia mgeni rasmi uzinduzi CEAT

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Umoja wa Kampuni za Kichina (CEAT) nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Umoja hu,o Shi Yong, alisema kuwa umoja huo ni muunganiko wa kampuni 72 za Kichina ambayo yanayofanya kazi hapa nchini katika sekta mbalimbali.

Rais huyo alizitaja sekta hizo kuwa ni kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, ikiwemo mwendokasi awamu ya 2 na ya 3, madaraja (Wami), viwanja vya ndege (Iringa), miundombinu ya maji (Kidunda mkoani Morogoro), upanuzi wa Bandari za Tanga, Dar es Salaam na ya uvuvi ya Kilwa.

Miradi mingine ipo kwenye sekta ya uchimbaji madini, kilimo ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.

Yong, alisema kuwa kuanzishwa kwa umoja huu utasaidia sana kuwa jukwaa ambalo litakuwa likitumika katika kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo utendaji wa kazi kwa makumpuni hayo yanayofanya kazi hapa nchini.

Aidha, Rais Yong alisema kuwa kampuni nyingi za Kichina hapa nchini ndiyo ambayo yanaongoza katika utoaji wa ajira kwa wingi kwa vijana wa Kitanzania wanaofanya kazi katika kampuni hizo.

Kuanzishwa kwa umoja huo ni kielelezo cha ushirikiano wa muda mrefu wa kirafiki kati ya hayati Rais Mao Tse Tung wa Jamhuri ya Watu wa China na hayati Rais Julius Nyerere wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button