Samia: Nimekuja Zambia tuimarishe uchumi

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema amekwenda kufanya ziara nchini Zambia ili nchi hizo ziimarishe uchumi.

Alisema hayo wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Zambia kabla ya kuondoka kurudi nyumbani jana jioni.

Rais Samia alisema ushirikiano wa Tanzania na Zambia pia unaimarishwa kupitia miundombinu iliyojengwa kuunganisha nchi hizo ikiwemo barabara kuu ya Tanzania-Zambia (Tanzam), Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama) na safari za ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) nchini humo.

“Nimekuja Zambia kuimarisha nia yetu ya kufanya kazi pamoja ili kuimarisha ushirikiano wetu wa kiuchumi,” alisema.

Rais Samia alisema reli ya Tazara hiyo inasafirisha mizigo tani za ujazo 210,000 kwa mwaka hivyo jitihada zinahitajika ili reli hiyo kutumika kwa uwezo wake wote.

Pia alisema uwezo wa Tazara ni kusafirisha watu milioni tatu kwa mwaka lakini kwa sasa inasafirisha watu 564,000 tu kwa mwaka.

“Serikali zetu mbili zinatambua umuhimu wa Tazara kwa uchumi wetu, hivyo jitihada zinahitajika kutatua changamoto ambazo zinaikabili reli hii,” alisema Rais Samia.

Kuhusu Bomba la Mafuta la Tazama, alisema mpango wa kulipanua ni muhimu kwa usalama wa nishati nchini Zambia hivyo Tanzania na Zambia zitaendelea kushirikiana katika mradi wa upanuzi.

Rais Samia alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na Zambia kutafuta rasilimali za kufadhili uboreshaji wa barabara kuu ya Tanzam ambayo ni muhimu katika kukuza biashara baina ya nchi hizo.

Alisema wabunge wa nchi zote mbili wana mchango katika kuhakikisha ushirikiano wa nchi hizo unaimarika.

Pia Rais Samia alisema kuna haja Tanzania na Zambia wavifanyie kazi vikwazo vya kibiashara visivyo vya kikodi na kuondoa urasimu ili kurahisisha biashara.

Pia alisema kiwango cha biashara kati ya Tanzania na Zambia kinazidi kuongezeka na kuna fursa ya kufanya biashara zaidi kutokana na uboreshaji uliofanywa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia aliwaeleza wabunge hao kuwa Serikali ya Tanzania imetoa hekta 20 kwa Serikali ya Zambia katika eneo la bandari kavu Kwala mkoani Pwani ili liendelezwe kwa ajili ya kuhifadhi mizigo ya nchi hiyo kwa muda mrefu wa siku 45 kutoka siku 15 za sasa katika Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema Tanzania pia imeanzisha mfumo wa dirisha moja la huduma kielektroniki kwa ajili ya kuhudumia wateja kwa haraka lakini pia muda wa Wazambia kuishi nchini bila viza umeongezwa kutoka siku 90 hadi siku 190.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Marry
Marry
1 month ago

Surprising! I’ve been making 100 Dollars an hour since I started freelance on the Internet six months ago. I work long hours a day from home and do the basic work that I get from the business I met online. share this work for you opportunity This is definitely the best job I have ever done………


…Go To This Link…………… > > > > http://Www.Smartcareer1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x