Samia: Simamieni sera kuendeleza rasilimali watu

DAR ES SALAAM: Rais, Samia  Suluhu Hassan amesema katika  kuisimamia vyema sera ya kuendeleza rasilimali watu ni vyema wanafunzi wanaofaulu na wale wanaofeli kutambuliwa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Desemba 16, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani Tanzania ( NECTA) jijini Dar es Salaam.

Amesema kwasasa NECTA inafanya kazi nzuri ya kuwatambua tu wale wanaofaulu katika mitihani yao na sera yao imewasahau wale wanaofeli kitu ambacho Rais Samia amesema kinakwamisha utekelezaji wa sera ya uendelezaji wa rasilimali watu.

Advertisement

“Wale wanaotoka na zero tunawatupa wapi? tunawafanya nini? sasa hawa tusipowashughulikia ndio ile sera ya uendelezaji rasilimali watu hatuitekelezi vizuri.” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi ameongeza kuwa ameridhishwa na mipango  ya Necta kuamua kuja na njia mpya za kumtathimini mwanafunzi ili kusaidia kuwekwa kwa mipango ya kuwaendeleza.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *