Samia: Tuangalie tulipojikwaa mmomonyoko wa maadili

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi kuangalia sehemu waliyokosea kwenye suala la malezi ya watoto na kulifanyia kazi suala hilo ikiwemo kuzingatia mira na desturi ili kuepuka mmomonyoko wa maadili.

Rais Samia amesema hayo leo Machi 8, 2023 wakati akizungumza kwenye Kongamano la Siku ya Wanawake wa Chadema lililofanyika mkoani Kilimanjaro na kuhudhuria viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe.

“Kuna mengine ya kuletewa tukatae yale ya kuletewa, sisi kama taifa tukatae yale yakuletewa, kwasababu yakija hayamuumizi mmoja, leo yamemuumiza jirani kesho yataingia kwako”.amesisitiza Rais Samia.

Aidha ameshauri wazazi kuhakikisha watoto wao wanawapa mafunzo ya dini ili kuepukana na mmomonyoko huo wa maadili.

Rais Samia ameshauri viongozi wa dini, serikali kuungana kwa pamoja na kuona nini cha kufanya katika kulinda maadili ikiwemo kuzilinda mila na desturi

Habari Zifananazo

Back to top button