Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema Tume ya Uchaguzi iko njiani kurekebisha Sheria ya Uchaguzi.
“Tutakapofikia hatua fulani za marekebisho tutakaa pamoja kuchambua kuona tunaendaje,” alisema na kuongeza kuwa pia kutafanyika marekebisho ya sheria mbalimbali ambayo yataelezwa na Waziri mwenye dhama ya Sheria na Katiba.
Rais Dk Samia amezungumza hayo leo Januari 3, 2023 wakati akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.