Samia: Tunazingatia utawala wa sheria

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema demokrasia imekuwa nyenzo muhimu kwenye uongozi wake kwa kuzingatia kuwa serikali anayoiongoza imekuwa ikitambua utawala wa sheria.

Rais Samia amezungumza hayo leo Machi 30, 2023 katika Ikulu ya Magogoni Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris.

“Suala la Demokrasia limekuwa muhimu sana kwenye serikali yangu, tumejitahidi kuwa serikali inayozingatia utawala wa sharia.”amesema Rais Samia.

Aidha, Makamu wa Rais, Kamala Harris amesifu demokrasia iliyopo nchini chini ya uongozi wa Rais Samia na kwamba Rais wa Marekani, Joe Biden anampongeza kutokana na hilo.

Marekani itaendelea kufanya kazi pamoja na utawala wa kidemokrasia katika kuunga mkono matakwa ya kidemokrasia na matakwa ya serikali hasa ya watu wa nchi hii,”

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x