Samia: Tutaelewana tu kama Katiba mpya au marekebisho

Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba kwa namna watakavyokubaliana na vyama vingine vya siasa.

Akizungumza na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 3, 2023, Rais Samia amesema kamati kadhaa zitafanya masuala mbalimbali kujua wapi pa kuanzia.

“Kuna haja ya kuangalia hali halisi ya sasa hivi, je yale yaliyomo mule mangapi yanatufaa na mangapi hayatufai, tunakwendaje,” amesema Rais Dk Samia.

Advertisement

Amesema wapo wanaotaka marekebisho ya Katiba na wengine wanataka mchakato wa katiba mpya na kwamba muda wowote kuanzia sasa itaundwa kamati ambayo itashauri namna ya kuendesha mchakato huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *