Samia: Tutaendelea kuwaunga mkono Yanga

DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza Yanga SC na kuahidi kuiunga mkono timu hiyo baada ya kuonesha mchezo mzuri katika mchezo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, Rais Samia amesema timu hiyo imeonesha kiu na juhudi ya kuiletea heshima taifa.

“Tunatarajia makubwa zaidi kutoka kwenu kwenye mashindano haya (Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho
la Soka Afrika) msimu ujao,”Tutaendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha,” amesema Mkuu huyo wa Nchi.

Yanga wakiwa ugenini katika mchezo uliomalizika usiku wa Aprili 05, 2024 wametolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti (3-2) baada ya mchezo wa ugenini jijini Pretoria kumalizika kwa sare tasa kama ilivyokuwa katika mchezo wa awali Machi 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button