GEITA. Bukombe. RAIS Samia Suluhu Hassan amewaeleza walimu nchini kuwa atahakikisha anashughulikia kero na changamoto zote zinazowakabili, ili kuendeleza sekta ya elimu nchini.
Rais Dk Samia amesema hayo leo Oktoba 6, 2023, alipozungumza kwa njia ya simu na walimu waliohudhuria hafla ya Siku ya Walimu duniani inayoadhimishwa kitaifa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kitaifa wakiongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko na mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita ipo kazini na ndio maana tayari imeshatatua baadhi ya changamoto za muda mrefu za walimu na inaendelea kushughulikia changamoto zingine zinazowakabili.
Amemuagiza Naibu Waziri Mkuu, Dk Biteko kuzungumza na kuwasikiliza walimu na kisha kumwasilishia maombi ya walimu, ili aweze kuyafanyia kazi na kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira rafiki
Comments are closed.