Samia: Yanga mmetuheshimisha

“MMEANDIKA historia jalili. Mmetuheshimisha sana. Hamasa yangu inaendelea na sasa imeongezeka. Kaifanyeni kazi,”ameandika Rais wa Tanzania, Samia Suluhu akielekezea klabu ya Yanga kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Rais Samia ameandika ujumbe huo leo Mei 2, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Ameipongeza timu hiyo kwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo na kuwatakia maandalizi mema katika mchezo ujao dhidi ya Marumo Gallants F.C.

Jumapili ya Aprili 30,2023 Yanga iliingia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuiondoa Rivers United ya Nigeria kwa jumla ya mabao 2-0.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button