Samia: Mazao ya korosho, ufuta na mbaazi yanalipa

LINDI,Mtama: Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima wa Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi kuzalisha kwa wingi mazao ya korosho, ufuta na mbaazi kwani soko la bidhaa hizo kwa sasa ni kubwa na la uhakika.
Hayo ameyasema leo Septemba 18, 2023 akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara, ambapo Rais amesema ili kuhakikisha biashara ina shamiri mkoani humo, ni lazima wananchi wadumishe hali ya amani na utulivu.
“La kwanza, ninawaomba sana kaeni kwa usalama, kwasababu mkitulia sisi tunapata wasaa wa kuangalia tuelekee wapi tutafute fedha wapi na wapi tupeleke nini mkichafuana mnatupa kazi nyingine ya kufanya,
Tuwaombe sana mkae kwa amani na utulivu na Mungu awabariki sana la pili kama mlivyoona mwaka huu na Mbunge amesema hapa Ufuta, Mbaazi bei imekwenda juu nataka niwahakikishie tunahangaika na Waziri wa Kilimo, (Hussein Bashe) kuhakikisha kwamba korosho nayo inakwenda kupanda bei lakini ili korosho ipande bei kuna mambo lazima tufanye, lazima tuongeze thamani kwenye korosho tunayoivuna,” amesema Dk. Samia.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *