Samsung, Tigo waiunga mkono Serikali huduma 5G

KATIKA kuendelea kuiunga mkono Serikali kwenye masuala ya teknolojia, kampuni ya simu Samsung na kampuni ya huduma za mawasiliano Tigo zimekuja na simu maalum yenye uwezo wa 5G.

Septemba Mosi,2022 jijini Da es Salaam, Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alishuhudia zoezi la uzinduzi wa teknolojia ya 5G ikiwa ni jitihada za Serikali kukuza teknolojia nchini.

Mkurugenzi wa Tigo – Kaskazini, Henry Kinabo alisema: “Kwa ushirikiano na Samsung, ushirikiano wetu katika kutambulisha simu ya Galaxy S24 unathibitisha dhamira yetu ya kutoa vifaa vya hali ya juu kwa wateja wetu.”

Advertisement

Amesema kampuni hiyo tangu mwaka 2022, imewekeza zaidi ya Sh trilioni 1 za Kitanzania lengo ni kufikia wigo wa 4G kote nchini na kutekeleza 5G katika vituo vikuu vya mijini ifikapo mwisho wa 2024.

“Ni muhimu kufahamu kuwa, uwekezaji wa Tigo katika kuboresha miundombinu yake ya mtandao umepata kutambuliwa kimataifa, ambapo Ookla imethibitisha Tigo kuwa mtandao wa kasi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2023,”

Aidha, katika ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa robo ya nne ya mwaka 2023, Tigo ilishika nafasi ya kwanza kwa ubora wa huduma. Hii inamaanisha kuwa, wateja wetu wanaonunua simu mbalimbali za Galaxy S24 wanaweza kufurahia huduma bora”. Amesema.

(Kushot -Kulia) Henry Kinabo, Mkurugenzi wa Tigo – Kaskazini akiwa na Edwin Byampanju, mwakilishi wa Samsung Tanzania  katika uzinduzi wat oleo jipya la Galaxy S24 katika Viwanja vya Ushhirika, Moshi.