Sanaa ni kichocheo cha kujenga mahusiano

DAR ES SALAAM: Maonesho ya michoro ya maandishi “kaligraphy” yamefunguliwa Novemba 21- 26 jijini Dar es salaam kikundi cha Albayrak Group.

Ni wiki muhimu kwa wasanii wachoraji wa maandishi ndani na nje ya nchi kwaajili ya kuonesha kazi zao za sanaa.

Naibu Spika Baraza la Wawakilishi Zanizbar, Mgeni Hassan Juma amesema kuwa sanaa ni njia moja ya kutambuana hivyo hutoa fursa ya kuheshimiana, tamaduni tofauti hupelekea kujenga mahusiano ya kibinaadam yanayosaidia kujenga amani na maelewano.

Advertisement

“” kubadilishana tamaduni ni njia moja wapo ya kutambuana, kila moja kati yetu ana utamaduni wake, tunapojifunza tamaduni za wengine inamaana tunaanza kujenga mahusiano ya kibinaadam yanasadia kuishi katika dunia yenye amani na mshikamano” amesema Mgeni

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya Shirika la Uturuki TIKA lilosimamia ufadhili wa onesho hilo amesema wataendelea kutumia sanaa kutunza umoja na mshikamano sio tu baina ya Tanzania na Uturuki pamoja na sehemu zingine duniani.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji bodi ya filamu Tanzania Dk Kiagho Kilonzo ameeleza nia ya Uturuki kuongeza mahusiano na Tanzania ya kitaaluma upande wa filamu kwa kutoa mafunzo ya filamu na ufundi kwa Watanzania ikizingatiwa  Uturuki ni nchi inayofanya vizuri kwenye tasnia hiyo

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *