Sancho ajiunga Dortmund

KLABU ya Borrusia Dortmund imemrudisha kwa mkopo winga wa Man United, Jadon Sancho.

Sancho amerejea Bundasliga miaka miwili na nusu badaa ya kujiunga na United kwa dau la Pauni milioni 73, lakini hakucheza tangu Agosti 2023 baada ya kukwaruzana na kocha wake Eric Ten Hag.

Mkataba wa Sancho Old Trafford unamalizika 2026, huku akiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.

Kabla ya kujiunga na United, Sancho alifunga mabao 50 an kutoa pasi za mabao 64 katika michezo 137 akiwa na Dortmund.

Habari Zifananazo

Back to top button