Sancho atengwa kikosi cha kwanza

SAKATA la mshambuliaji wa Manchester United, Jadon Sancho dhidi ya kocha wake Eric Ten Hag limechukuwa sura mpya baada ya leo timu hiyo kutoa kauli dhidi ya Muingereza huyo.

United imesema kuanzia sasa mshambuliaji huyo wa zamani wa Borrusia Dortmund hatofanya mazoezi na kikosi cha kwanza badala yake amepewa programu maalumu ya mazoezi.

“Jadon Sancho atabaki na program maalum ya mazoezi binafsi, nje ya kikosi cha kwanza, hilo kutokana na masuala ya kinidhamu.” imeeleza taarifa hiyo.

Wiki iliyopita kocha Eric Ten Hag alisema Sancho hatumiki kwenye michezo ya hivi karibuni kwakuwa amepewa programu maalum iliyotokana na kiwango chake kisichoridhisha mazoezini, hata hivyo mchezaji huyo alikanusha taarifa hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button