Sangoma mbaroni akidaiwa kubaka makaburini

Sangoma mbaroni akidaiwa kubaka makaburini

JESHI la Polisi mkoani Mtwara, linamshikilia mganga wa Kienyeji  Sabihi Issa Mpando, mwenye umri wa miaka 41, mkazi wa Chipuputa manispaa ya Mtwara Mikindani  akidaiwa kumbaka binti wa miaka 17, makaburini.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa alitumia mbinu ya kumlaghai kumpa matibabu binti huyo kwa masharti ya kumuingilia kimwili makaburini, huku akimweleza kuwa ni tiba.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Hamisi Ramadhani  amethibisha kutokea kwa tukio na kufafanua kuwa limetokea Februari 23,2023 majira ya usiku katika eneo la makaburi ya Mingano.

Advertisement

Jeshi la Polisi limesema limebaini chanzo cha tukio hilo ni tamaa za mwili na kujistarehesha na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo.

/* */