Sawa Morocco kafungwa ila hadaiwi!

Soccer Football - FIFA World Cup Qatar 2022 - Fans in Casablanca watch France v Morocco - Casablanca, Morocco - December 14, 2022 A Morocco fan reacts as they watch the match REUTERS/Silvio Castellanos

JUMATANO jioni kwenye Uwanja wa Al Bayt ulikuwa ni sehemu ya ndoto kwa Morocco kufika fainali ya Kombe la Dunia, lakini wanasema jitihada haziwezi kuzidi mipango ya Mungu.-

Mashabiki kote ulimwenguni, na sio Wamorocco pekee, walikuwa wamebofya vitufe vyao vya kusinzia ili kuruhusu ndoto hiyo kudumu kwa muda mrefu zaidi, wakiiweka kwa dakika 90, lakini waliamka bila mafanikio.

Morocco ilikuwa tayari imevuka matarajio kwa kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia huko Qatar 2022, ikizishinda Ubelgiji, Canada, Uhispania na Ureno.-

Advertisement

Tangu kuifunga Ubelgiji, Morocco ilitarajia kufuzu hatua ya 16 bora. Matarajio yaliongezeka walipoishinda Uhispania. Ndoto iliacha imani baada ya kuifunga Ureno.-

Wataalamu wa kifaransa walihakikisha Simba wa Atlas hawamalizi nafasi ingine zaidi ya mshindi wa tatu. Hakika imewaumiza Wamorocco, baadhi ya mashabiki wanaeleza namna walivyoumizwa na kushindwa kwao.-

“Huu ni mpira, ndivyo unavyofanya kazi,” Fatima anasema shabiki wa Morocco. Tunajivunia na timu,soka la Morocco limebadilika kwa sasa, hatujapoteza hakuna namna, ila sisi ni mabingwa.”

-Kipenga cha mwisho kilipopulizwa na Ufaransa kushinda mabao 2-0, wachezaji wa Morocco walikusanyika na kutoa heshima zao kwa mashabiki wao huku Ufaransa ilisherehekea fainali yao ya pili mfululizo.

-“Tunajivunia ndivyo ninavyojisikia kwa sasa, Amine, shabiki mwingine wa Morocco anasema. “Tumeandika historia bado vijana, na sasa wana matarajio kwa mashindano yajayo, hatutakata tama,” anaongeza.-

“Kwa upande mwingine nimeumizwa sana” anasema shabiki huyo. Imekuwa safari ya kuvutia, tuna furaha na kujivunia, tutawaunga mkono mpaka mwisho.”-

“Tunajivunia na Simba wa Atlas” anasema Lamia. “Hakuna hata mmoja kati yetu aliota kwamba tungeweza kufika nusu fainali, kiukweli tunataka kushinda nafasi ya tatu, ila ni sawa tu hata isipotokea, tayari tumeshafanya zaidi ya tulivyokuwa tunatarajia.”

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *