Sawadogo ndo basi Msimbazi

SIMBA SC imetangaza kuachana na kiungo wao Ismael Sawadogo kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.

Maamuzi hayo ni mwendelezo wa kuwapa mkono wa kwaheri baadhi ya wachezaji ambao hawapo kwenye mipango ya timu hiyo msimu ujao.

Taarifa za Simba SC kuachana na kiungo huyo mkabaji zimetolewa na timu hiyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Mpaka sasa Simba SC ishaachana na Mohammed Ouatarra, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Nelson Okwa, Beno Kakolanya na Victor Akpan.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button