SBL yawezesha wengi kupata maji

Wakati dunia inaadhimisha siku ya maji duniani leo hii, hali bado inatia mashaka kwamba bado mamilioni ya watu duniani hawajafikiwa na maji safi na salama.

Hata hivyo, nchini Tanzania, kuna matumaini kwani serikali inaendelea kufanya hatua muhimu kutimiza lengo lake la kutoa maji safi na salama kwa asilimia 85 ya wakazi wa vijijini na asilimia 95 ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2025.

Kwa Serengeti Breweries Ltd (SBL), maji si tu ni kipengele muhimu; ni rasilimali kubwa sana inayotumika katikati ya mahitaji yanayoongezeka kila kukicha duniani. Hivyo basi, ndani ya mpango wake wa miaka kumi wenye jina la ‘Society 2030: Spirit of Progress’ wamelenga kuchukua hatua za kutunza mazingira, ustawi wa jamii, na utawala (ESG). Lengo ni kujenga jamii inayoshirikishwa, jumuishi na endelevu.

Wakati SBL inajikita kwenye lengo hili, uhifadhi wa maji kwa ajili ya ustawi wa jamii inaendelea kuwa sehemu kuu ya ahadi yake ya kuchochea jamii endelevu.

SBL imechukua hatua kadhaa za kijamii kwa kuanzisha miradi ya maji ambayo kwa pamoja inatoa maji safi na salama kwa mamilioni ya Watanzania. Tangu mwaka 2010, SBL imewekeza zaidi ya TZS bilioni 2 katika miradi 25 ya maji nchi nzima kupitia mpango wao wa kuokoa maisha ya watu kupitia miradi hii ya maji ambayo inalenga jamii maskini za vijijini wanaotembea umbali mrefu kuchota maji kwenye mabwawa na mito.

Kwa kushirikiana na mashirika kama WaterAid na AMREF, SBL imehakikisha kuwa hata maeneo yenye uhitaji mkubwa yanapata ufikiaji wa maji safi na salama.

Na kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa Kampuni ya SBL, John Wanyancha alisema, “Dhamira ya SBL kwa ustawi wa jamii inathibitishwa na program yetu ya Water of Life ambapo ni moja ya maeneo yetu manne ya kipaumbele yanayolenga kuboresha ustawi wa kijamii nchini Tanzania.”

Zaidi ya hayo, Wanyancha alisema kuwa kampuni inatekeleza usimamzi bora wa miradi ya maji katika maeneo yenye shughuli zake. Kutokana na kwamba zaidi ya 90% ya bia na 60% ya vilevi vinatengenezwa hutokana na maji hivyo kupunguza matumizi ya maji ni muhimu kwa uhifadhi wa maji. Katika hali hiyo, ndani ya miaka mitatu iliyopita, SBL imepunguza uwiano wa matumizi ya maji kwa 15.6%, ikiiokoa karibu lita milioni 80 za maji. Baadhi ya sababu zilizochangia kwenye mafanikio haya ni pamoja na usimamizi bora, ufanisi mzuri, na utunzaji wa mali na matumizi ya teknolojia za kisasa.

Katika usimamizi wa taka, ahadi inaendelea kwenye matibabu sahihi ya maji taka katika maeneo yake, ambapo viwanda vya Dar es Salaam na Mwanza vinaendesha jitihada za kutibu maji taka, ikihakikisha maji taka yanakidhi viwango vya kisheria kabla ya kuyatoa nje. Kwenye kiwanda cha Moshi, maji taka hutibiwa kwenye kituo kinachosimamiwa na manispaa.

Aidha, SBL inaendelea kudumisha miundombinu yake wa mfumo wa maji ya mvua huku ikifuatilia kwa ukaribu ubora wa maji taka yanayotolewa ili kuhakikisha wanazingatia sheria zilizowekwa.

Halikadhalika, SBL inatambua umuhimu wa kushughulikia maswala yanayohusiana na maji katika minyororo yake ya usambazaji. Kutoka katika upatikanaji wa malighafi hadi utengenezaji na usambazaji, maji yana mchango muhimu katika shughuli zake za kibiashara.

SBL inashirikiana kwa karibu na wazalishaji kukuza ya usimamizi wa maji na kuhakikisha kwamba shughuli zinazotumia maji kwa wingi zinafanyika kwa njia endelevu. Kwa kushirikiana na washirika hawa, SBL inalenga kukuza utamaduni wa utunzaji wa maji na kuhamasisha washirika wake wanazingatia taratibu hizi.

Katika kutambua thamani ya kulinda rasilimali za maji kwa shughuli zake, SBL imeenda mbali zaidi ya kuhimiza sera na tabia zinazopelekea uendelevu wa maji kwa kiwango kikubwa na kwa jamii zilizo kwenye hatari ya kuathirika zaidi.

SBL imekuwa ikifanya kazi kikamilifu na viongozi wa serikali, wadau wa viwanda, na vikundi vya uhamasishaji ili kuongeza ufahamu kuhusu changamoto za maji na kuleta masuluhisho sahihi. Kwa kutumia ushawishi na ujuzi wao, SBL inalenga kuleta mabadiliko chanya na kuchangia katika juhudi za kulinda rasilimali za maji kwa vizazi vijavyo.

Katika jitihada za kuimarisha ufikiaji wa wanawake kwenye huduma muhimu za maji, na usafi wa mazingira, SBL imeongeza juhudi zake kufuatana na jitihada za serikali za kuboresha ufikiaji wa maji safi na salama vijijini.

Kupitia ushirikiano na Africa Community Advancement Initiative (AFRIcai), SBL ilizindua mradi wa maji wa Kabila katika Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza, ukiwanufaisha watu 11,927 katika vijiji vitano: Ilambu, Mlimani, Igogo, Shuleni, na Majengo.

Mradi huu unalenga kuondoa ukosefu wa maji na kuboresha ustawi wa jamii. Aidha, SBL na AFRIcai walitoa mafunzo ya ujasiriamali, usimamizi wa fedha, na usafi ili kuwawezesha wanawake katika eneo hilo. Wakati huo huo, mradi mwengine wa maji unaendelea huko Mwanza unatarajiwa kukamilika mapema mwezi wa Aprili, ukiongeza zaidi ufikiaji wa maji safi katika eneo hilo.

Mmoja wa washiriki, Mary Mgaya kutoka kijiji cha Ilambu, alielezea shukrani zake kwa fursa hiyo: “Mafunzo yamenifungua macho kuhusu umuhimu wa maji safi na usafi. Sasa, siyo tu mnufaika; mimi ni mchangiaji mwenye shughuli katika ustawi wa jamii yangu.”

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameipongeza Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa msaada wake katika kufadhili miradi ya maji inayolenga kutoa maji safi na salama bure kwa watanzania katika maeneo ya vijijini yanayokabiliwa na uhaba wa maji, ambayo yanachangia juhudi za serikali za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama vijijini.

Habari Zifananazo

Back to top button