Sekondari Sinya yatakiwa kupanda miti

WAJUMBE wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha wameuagiza uongozi wa shule mpya ya sekondari Sinya iliyopo wilayani Longido kupanda miti maeneo yote ya shule ili kutunza mazingira.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha, Thomas ole Sabaya wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyojengwa na serikali kwa gharama ya Sh milioni 570.

Sabaya ameagiza uongozi wa shule hiyo chini ya mwalimu mkuu, Andrew Tekwin kupanda miti itakayozunguka maeneo yote ili kupata kivuli kwa walimu na wanafunzi kutokana na eneo hilo kuwa na vipindi vya joto wakati mwingi.

Awali, baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo akiwemo Juliana Saning’o waliishukuru serikali kwa kuwajengea shule hiyo ili kuleta chachu ya kusoma kwa jamii za kifugaji na jamii nyingine za maeneo ya pembezoni kutokana na jiografia ya eneo husika.

Habari Zifananazo

Back to top button