Senegal itatoboa leo 16 bora?

RAUNDI ya mwisho (3) ya michuano ya Kombe la Dunia inaanza leo, Timu ya Taifa ya Senegal inahitaji ushindi dhidi ya Ecuador ili kuingia kwenye hatua ya mtoano 16 bora. Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Khalifa saa 12;00 jioni.

Leo kutakuwa na michezo minne ya kundi A na B, mchezo wa pili wa kundi A utakuwa kati ya Uholanzi na Qatar, ambao utapigwa muda huohuo. Msimamo wa kundi hilo unaonyesha, Uholanzi anaongoza akiwa na pointi nne, sawa na Ecuador.

Senegal inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu, Qatar hawana pointi. Michezo mingine ya kundi B ni kati ya Wales na England, Iran na Marekani.

Katika kundi hilo, England anaongoza kwa pointi nne, Iran pointi tatu, Marekani pointi mbili, Wales pointi moja. England inahitaji sare kujihakikishia kufuzu hatua ya 16 bora, wakati Iran inahitaji sare au ushindi kuendelea na hatua hiyo. Michezo hiyo itapigwa saa 4:00 usiku.

Habari Zifananazo

Back to top button