TIMU ya Taifa ya Senegal leo itakuwa na kibarua kigumu cha kusaka nafasi ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia ambapo itachuana na England katika mchezo wa 16 bora utakaopigwa saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Al Bayt.
Senegal ndio timu pekee iliyoshinda katika majaribio tisa ya timu za Afrika katika michezo ya mtoano dhidi ya mataifa ya Ulaya, ikiishinda Sweden katika hatua 16 bora mwaka 2002 huku ikiwa na sababu za kujiamini baada ya kuzishinda Qatar na Ecuador na kumaliza nyuma ya Uholanzi katika Kundi A.
Historia ya England dhidi ya Senegal
Hii itakuwa mechi ya kwanza ya kimataifa kati ya England na Senegal.
Senegal wako katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili, awali walifanya hivyo mara yao ya kwanza mwaka 2002, walipotinga robo fainali.
Ushindi dhidi ya Qatar na Ecuador katika hatua ya makundi pia unamaanisha kuwa Senegal imeshinda mechi mfululizo za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
Rekodi ya England dhidi ya timu za Afrika
Bahati waliyonayo England dhidi ya timu za Afrika inawapa matumaini na kuipa Senegal motisha ya kuandikisha historia.
Katika mechi 20 za hatua ya mtoano England imeshinda michezo 14 na kutoka sare sita hakuna rekodi ya kutopoteza. Mara ya mwisho England iliifunga Ivory Coast mabao 3-0 huko Wembley mnamo Machi 2022, katika mchezo wa kirafiki.
Haijakuwa kuwa rahisi Kombe la Dunia, England imeshindwa kushinda mechi tatu kati ya saba dhidi ya timu za Afrika kwa dakika 90.
Katika robo fainali ya 1990, zilibaki dakika saba tu, Uingereza itolewe na Cameroon iingine nusu fainali, lakini mshambuliaji Gary Lineker alipiga penalty iliyofanya matokeo kuwa 2-2 na Cameroon kutolewa kwa mabao 3-2 baada ya dakika 30 za nyongeza.
Hii ni orodha ya matukio ambayo England wamekutana na upinzani wa Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia ambazo bado hawajapoteza.
Date | Stage | Result/Fixture | Stadium |
June 6, 1986 | Group | 0-0 vs. Morocco | Estadio Tecnologico, Mexico |
June 21, 1990 | Group | 1-0 vs. Egypt | Stadio Sant’Elia, Italy |
July 1, 1990 | Quarterfinals | 3-2 vs. Cameroon | Stadio Diego Armando Maradona, Italy |
June 15, 1998 | Group | 2-0 vs. Tunisia | Stade Velodrome, France |
June 12, 2002 | Group | 0-0 vs. Nigeria | Yanmar Stadium Nagai, Japan |
June 18, 2010 | Group | 0-0 vs. Algeria | Cape Town Stadium, South Africa |
June 18, 2018 | Group | 2-1 vs. Tunisia | Volgograd Arena, Russia |
December 4, 2022 | Round of 16 | vs. Senegal | Al Bayt Stadium, Qatar |