Senegal yafuzu 16 bora Kombe la Dunia

YAMETIMIA!! Baada ya takribani miaka 20, hatimaye Senegal imefuzu hatua ya 16 bora ya mashindano ya Kombe la Dunia, kufuatiwa ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya Ecuador. Imekuwa timu ya kwanza Afrika kutinga hatua hiyo.

Mwaka 2002 Senegal ikiwa chini ya kocha mfaransa, Bruno Metsu walipita hatua hiyo hadi robo fainali na kupoteza mchezo bao 1-0 dhidi ya Uturuki, bao lililofungwa na Ilhan Mansiz mturuki mzaliwa wa Ujerumani.

Mabao ya Senegal yamefungwa na Ismail Sarr kwa penalty na Koulid Koulibaly kwa akiunganisha mpira wa kona.

Wakati bao la Ecuador likifungwa na Moise Caicedo kiungo kutoka Brighton Hove Albion ya England.

Kuanzia Kombe la Dunia la mwaka 2006 mpaka 2014, Senegal haikupata nafasi ya kufuzu, 2018 ilifuzu na kuishia hatua ya makundi, ambapo katika kundi H, Senegal ilipangwa na Colombia, Poland na Japan, na Senegal kumaliza akiwa na pointi nne.

Baada ya Senegal sasa, timu nne zimebaki kutoka Afrika, Morocco ambao wako kundi F wakiwa na pointi nne, sawa na vinara wa kundi hilo, Croatia, wengine ni Ghana mwenye pointi tatu katika kundi H, Ureno wakiongoza kwa pointi sita.

Kundi G Cameroon wana pointi moja, mchezo wa mwisho wanamaliza na Brazil, Tunisia wana pointi moja mchezo wa mwisho wanamaliza na Ufaransa

Habari Zifananazo

Back to top button