ZOEZI la Sensa ya Watu na Makazi kwa Mkoa wa Tanga limefikia asilimia 60 ya lengo, Mkuu wa Mkoa Omar Mgumba amesema wakati wa bonanza la kuhamasisha sensa lililoandaliwa na club ya waandishi wa habari mkoani hapo.
Amesema kuwa Mkoa umeendelea kufanya vizuri katika zoezi la sensa ambapo kutokana na kasi ya uandikishaji na uhamasishaji inavyoendelea wanatarajia kuvuka lengo .
“Niwaombe wenyeviti wa mitaa kutoa taarifa kwa wananchi siku ambayo karani wa sensa wataweza kupita kwenye maeneo yao Ili kutoa fursa ya kufanya shughuli za maendeleo badala ya kukaa kusubiri kuhesabiwa,”amesema RC Mgumba.
Mwenyekiti wa club ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Tanga Lulu George amesema kuwa wameamua kuandaa bonanza hilo Kwa ajili ya kuiunga mkono serikali kuhamasisha zoezi la sensa.
“Licha ya kutumia kalamu zetu katika kuhamasisha zoezi la sensa tumeamua kufanya bonanza la michezo mbalimbali Ili kupeleka ujumbe kwa wananchi kushiriki zoezi hili muhimu,” amesema George.