SENSA2022: DC Kahama akiri usumbufu kidogo nyumba za kulala wageni

Mkuu  wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga

MKUU  wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga  amesema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 linaendelea vizuri ingawa kulijitokeza usumbufu kidogo katika nyumba za kulala wageni hata hivyo wote wamehesabiwa.

Akitoa taarifa ya namna zoezi linavyoendelea katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Kiswaga amesema makarani wa sensa wameonesha umahiri katika kuelimisha umma na kwamba watu wameendelea kutoa ushirikiano chanya wa kuhesabiwa.

Advertisement

“Tulianza zoezi hili usiku wa saa sita hususani katika maeneo ya stendi, nyumba za kulala wageni na hospitalini,” amesema DC Kiswaga.

Vile vile DC Kiswaga amesema watu ambao wamehesabiwa na kwa bahati mbaya wakafariki bado taarifa zao zitachukuliwa. 

Pia unaweza soma: Afariki Dunia muda mchache baada ya kuhesabiwa

Mkazi wa kata ya Segese Halmashauri ya  Msalala wilayani Kahama Mponda Masele amekiri  kupigiwa  simu na karani wa sensa  nakutoa taarifa sababu mke wake hajui kujieleza vizuri.