SHIRIKA la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa limeipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Mtakwimu Mkuu kwa hatua ambayo imefikia hadi sasa katika zoezi la kuhesabu Watu na Makazi #Sensa2022.
UNFPA Tanzania imeandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuwa “Tunawapongeza NBS na OCGS kwa hatua kubwa ambazo tayari zimefikiwa katika #Sensa2022🇹🇿”
UN inafanya kazi kwa karibu na NBS & OCGS, na imekiri kuwa zoezi limekidhi viwango vyote muhimu vya kimataifa katika kufanya Sensa ya kidijitali yenye ubora na inayoaminika.