OFISI ya Taifa ya Takwimu NBS imesema asilimia 99.93 ya watu wamehesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 iliyoanza Agosti 23 na kusema asilimia iliyobaki itatimia kabla ya Septemba 5, 2022.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa amesema leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo. Amewataka wananchi ambao hawajahesabiwa kupiga simu zilizotolewa ili makarani wawafikie.